Social Icons

Pages

Featured Posts

Friday, October 7, 2016

Kundemba yatoka sare na Leeds katika mechi ya ufunguzi ya Daraja la Pili

 Kikosi kamili cha Timu ya Kundemba kilichofungua dimba katika Ligi ya Daraja la Pili kwa kumenyana Leeds. Matokeo hadi mwisho wa mpira hakuna mbabe 1-1.

Mchezaji wa timu ya Kundemba Kishtunda akiwa kazini

Tuesday, March 15, 2016

Kundemba yatoka sare na Sicco 2-2

 Baadhi ya wachezaji wa akiba wa Kundemba
 Msaidizi Kocha Ahmada Noma akiwapa maelekezo vijana wake kwenye mechi yao dhidi ya Sicco ambapo timu zilitoka sare 2-2
Leo Timu ya kundemba imeshindwa kuendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kutoka sare ya 2-2 na timu ya sicco  katika mchezo wa daraja la Pili uliofanyika jana kwenye viwanja vya Amaan.

Mpaka timu zinaenda mapumziko Kundemba ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 ndipo ilipofanya mabadiliko muhimu kwa kumtoa Haruob na kumuingiza Hafidh Gino  na baadae kumtoa Cabaye na nafasi yke kuchukuliwa na Rashid Kidishi.

Mabadiliko haya yalizaa matunda kwani dakika  ya 7 ya kipindi cha pili Rashid Kidish aliiandikia Kundemba bao la kwanza na dakika 10 baadae Hassan au Bamzu alisawazisha goli kwa kichwa baada ya kuunganisha Krosi iliyopigwa na Abdull ss 

Kundemba ina alama 16 ikiwa imebakiza michezo 3 

MUNGU IBARIKI KUNDEMBA

Sunday, February 28, 2016

Kundemba yaichapa Al Hilal 2-0

 Timu ya Kundemba imeendeleza kurudumu lake la ushindi wa mechi ya 3 mfululizo baada ya kuwachabanga al Hilal mabao 2-0 magoli jana 2/02/2016 hapo Uwanja Amaan ambayo yamewekwa kiamiani na Sadi Ambani Kapteni na Abdalla umaarufu dume.



Sunday, February 21, 2016

Kundemba Ikishangiria, We acha tu

Timu ya Kundemba ambayo ipo katika daraja la pili Wilaya ya mjini Unguja, ni mojawapo katika timu chache zilizo madaraja ya chini lakini huvuta hisia za wapenzi wengi wa mpira wa miguu kiasi cha kuchangamsha Uwanja na watazamaji kwa vionjo lakini pia kuwatia mori wachezaji wa Kundemba kwamba jukwaani wana mchezaji No 12 anawefuatilia kwa karibu na kuwapa sapoti. Hapa Kundemba ilikuwa ikicheza na Timu ya Gulioni, na wapenzi walitinga Uwanjani na Dufu kuwaunga mkono wachezaji.

Sunday, December 13, 2015

Kundemba V/S Amani Fresh


 Kikosi kamili cha timu ya Kundemba kilichomenyana na timu ya Amani Fresh hapo uwanja wa Jeshi Migombani. Kundemba ilipoteza mchezo huu kwa kufngwa bao 1-0

 Kikosi kamili cha timu ya Amani Fresh ambacho kiliibuka kidedea kwa kuifunga timu ya Kundemba 1-0 katika chezo wa ligi daraja la pili  tarehe 01/12/15


 Wachezaji wa Kundemba wakienda mapumzikoni baada ya kumalizika kipndi cha kwanza huku matokea yakiwa bado no 0-0

  Wachezaji wa Amani Fresh wakienda mapumzikoni baada ya kumalizika kipndi cha kwanza huku matokeo yakiwa bado no 0-0

Sunday, October 4, 2015

Kundemba yaanza vyema ligi daraja la pili yaifunga Rascazone 3-2



Timu ya kundemba leo imeanza mechi yake ya kwanza kwa ushindi wa magoli 3-2 Kundemba ilicheza na timu ya ras cazone ktk uwanja wa amaan mida ya 8:00 mchana magoli ya kundemba yalifungwa na sadi mgeni ambae kwa leo alikua captain yeye aweka kimiani magoli 2 yte kwa njia ya penalti na la 3 lilifungwa na ali abdalla umaarufu dume mnamo dakika za 85 ambaye alitokea bench


Mfungaji wa Goli la tatu Ali Abdalla 'dume' akishangilia baada uya kuwatungua Rascazone katika dakika ya 85