Social Icons

Pages

Tuesday, March 15, 2016

Kundemba yatoka sare na Sicco 2-2

 Baadhi ya wachezaji wa akiba wa Kundemba
 Msaidizi Kocha Ahmada Noma akiwapa maelekezo vijana wake kwenye mechi yao dhidi ya Sicco ambapo timu zilitoka sare 2-2
Leo Timu ya kundemba imeshindwa kuendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kutoka sare ya 2-2 na timu ya sicco  katika mchezo wa daraja la Pili uliofanyika jana kwenye viwanja vya Amaan.

Mpaka timu zinaenda mapumziko Kundemba ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 ndipo ilipofanya mabadiliko muhimu kwa kumtoa Haruob na kumuingiza Hafidh Gino  na baadae kumtoa Cabaye na nafasi yke kuchukuliwa na Rashid Kidishi.

Mabadiliko haya yalizaa matunda kwani dakika  ya 7 ya kipindi cha pili Rashid Kidish aliiandikia Kundemba bao la kwanza na dakika 10 baadae Hassan au Bamzu alisawazisha goli kwa kichwa baada ya kuunganisha Krosi iliyopigwa na Abdull ss 

Kundemba ina alama 16 ikiwa imebakiza michezo 3 

MUNGU IBARIKI KUNDEMBA